Skip to main content

Utatuzi wa Migogoro

Mgogoro maana yake ni:-

(a) Mgogoro wa maslahi kama pande za kwenye mgogoro zinajishughulisha na huduma muhimu:

(b) Ni malalamiko kuhusu –

(i) haki au uhalali wa kisheria; (ii) kukiukwa kwingine kwa Sheria hii au kuvunjwa kwa mkataba;

Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Mwenendo au Usuluhishi

Pande mbili katika mkataba zinaweza kukaa pamoja mezani na kusuluhisha mgogoro baina yao. Kama pande zitashindwa kutatua mgogoro baina yao, hawatafungwa kupeleka mgogoro huo kwa msuluhishi au Tume ya Usuluhishi kama itakavyo kuwa inaonyeshwa kwenye mkataba wao.

Msuluhishi pamoja na pande zote kwenye mgororo watafanya yafuatayo:-

  • kuamua muda, tarehe na mahali pa kusikiliza usuluhishi; na
  • kuzishauri pande zilizo kwenye mgogoro juu ya maelekezo ya mgogoro huo.

Pia  Msuluhishi –

  • anaweza kuendesha usuluhishi katika jinsi ambayo msuluhishi ataona kuwa inafaa kwa ajili ya kuamua mgogoro kwa haki na kwa haraka;
  • atatakiwa kushughulikia undani wa mgogoro bila kujali sana taratibu za kisheria;

Kwa kuzingatia utashi wa msuluhishi juu ya mfumo mzuri wa mwenendo, upande kwenye mgogoro unaweza kutoa ushahidikuita mashahidikuuliza mashahidi na kutoa hoja.

Kama pande zilizo kwenye mgogoro zitakubali, msuluhishi anaweza kuahirisha mwenendo na kutatua mgogoro kwa njia ya upatanishi.

Katika kila usikilizaji wa usuluhishi upande ulio kwenye mgogoro unaweza kuwakilishwa na –

  • wakili; au
  • mwakilishi binafsi ambaye upande utamchagua.

Mwisho: Msuluhishi anaweza kutoa tuzo inayofaa lakini hawezi kuamuru gharama isipokuwa kama upande au mtu anayewakisha upande alitenda kwa nia mbaya au kwa uchokozi.

Ndani ya siku thelathini za kuhitimishwa kwa mwenendo wa usuluhishi, msuluhishi analazimika kutoa tuzo na sababu iliyosainiwa na msuluhishi.

 

MOTOKEO YA TUZO YA USULUHISHI

Tuzo ya msuluhishi iliyotolewa chini ya Sheria itawabana pande zote kwenye mgogoro.

Tuzo ya usuluhishi iliyotolewa chini ya Sheria inaweza kupelekwa na kutekelezwa katika Mahakama husika kama vile ni amri ya mahakama ya sheria.

Masahihisho ya tuzo ya usuluhishi

Msuluhishi ambaye ametoa tuzo ya usuluhishi kwa mujibu wa sheria anaweza, kwa maombi au kwa utashi wake, kusahihisha kwenye tuzo kosa lolote la kuiandishi linalotokana na kuacha au kurukwa kwa bahati mbaya.

Mapitio ya tuzo ya usuluhishi

Upande wowote kwenye tuzo ya usuluhishi iliyotolewa, ambaye anadai kuwa kuna kosa lolote kwenye mwenendo wa usuluhishi anaweza, kuiomba Mahakama kutoa uamuzi mpya na kutipilia mbali tuzo ya usuluhishi, kwa kuzingatia yafuatayo:-

  • ndani ya wiki sita kuanzia tarehe mwombaji alipopelekewa tuzo isipokuwa kama kosa linalodaiwa linahusisha mwenendo mbaya;
  • kama kosa linalodaiwa linahusisha mwenendo mbaya, ndani ya wiki sita kuanzia pale mwombaji alipogundua kosa.

Hivyo basi; Mahakama inaweza kutupilia mbali tuzo ya usuluhishi iliyofanywa kwa sababu zifuatazo:–

  • kulikuwa na mwenendo mbaya kwa upande wa msuluhishi;
  • tuzo ilitolewa bila kufuata utaratibu.

Mahakama inaweza kuzuia utekelezaji wa tuzo ili kusubiri uamuzi mpya kama tuzo ya usuluhishi itakuwa imetupiliwa mbali. Kama tuzo imetupiliwa mbali Mahakama ya Kazi inaweza:-

  • kuamua mgogoro katika namna ambayo inaona inafaa;
  • kutoa amri yoyote ambayo inaona inafaa juu ya utaratibu utakaofuatwa ili kuamua mgogoro.

Angalizo: Matumizi ya Sheria ya Usuluhishi Sura ya 15, haitatumika katika usuluhishi utakaoendeshwa na Tume.

MAHAKAMA

Makubaliano ya kuzuia mwenendo wa mahakama ni batili. Kifungu cha 28 cha Sheria ya Mikataba; Makubaliano yote, ambayo mhusika yeyote anazuiwa kudai haki yake chini ya mkataba kwa utaratibu wa kawaida wa mahakama, au yanayopunguza muda wa mhusika kudai haki hiyo, ni batili kwa kiasi hicho:

Isipokuwa kwamba kifungu hiki –

(a) hakitasababisha uharamu wa –

(i) mkataba ambao watu wawili au zaidi wamekubaliana kwamba mgogoro wowote utakaotokea baina yao utapelekwa kwenye usuluishi, na kwamba kiasi kile tu kitakachotolewa kwenye usuluhishi ndicho kitakacholipwa kuhusiana na mgogoro huo; au

(ii) mkataba wowote ulio katika maandishi ambao watu wawili au zaidi wamekubaliana kupeleka kwenye usuluishi swali lolote baina yao ambalo limekwisha jitokeza; au

  • kuathiri kifungu chochote cha sheria yoyote inayotumika kuhusiana na usuluhishi.