Skip to main content

Ubia na Ushirika

Asili ya Ubia na Ushirika

“Ubia” ni uhusiano uliopo baina ya watu wanaofanya biashara kwa pamoja ambayo inazalisha faida.

Mtu aliyeingia ubia na mwingine wanaitwa kwa umoja wao “shirika”, na jina wanalolitumia kwenye biashara ni “jina la shirika”. (Kifundu cha 190 Sheria Namba 345)

KANUNI ZA KUJULISHA KUWEPO KWA UBIA

Mahusiano ya ubia yanatokana na mkataba na siyo wadhifa. Hiyo basi katika kuamua kama kundi la watu ni wabia au siyo, uzito utawekwa katika kanuni zifuatazo-

(a) upangaji wa pamoja, upangaji unaofanana, mali za pamoja, mali zinazofanana au umiliki wa sehemu tu hausababishi ubia kwa mali yoyote waliyonayo, iwe mpangaji au mmiliki wanagawana au la faida wanayoipata mahali pale;

(b) kugawana mapato ya mwisho pekee hakusababishi ubia, iwe wanaogawana mapato hayo wana haki za pamoja au la, au maslahi ya pamoja katika mali ambayo malipo ya mwisho yanatolewa;

(c) kupatikana kwa faida ya mtu mwenye hisa katika biashara ni ushahidi wa awali kuwa ni mbia katika biashara, lakini upatikanaji huo wa hisa au malipo yoyote kulingana na faida ya biashara, yenyewe peke yake hayamfanyi awe mbia katika biashara, na zaidi upatikanaji huo wa hisa au malipo-

(i) kwa kutoa mkopo kwa mtu aliyeingia au anayetegemea kuingia kwenye biashara;

(ii) kwa mtumishi au wakala kama ujira;

(iii) kwa mjane au mtoto wa marehemu mwenye ubia kama kiinua mgongo;

(iv) kwa mmiliki wa zamani au mmiliki wa sehemu ya biashara, kama malipo ya mauzo ya hisa, havimfanyi mpokeaji awe mbia na mtu anayefanya biashara.

MAHUSIANO BAINA YA WABIA

Wabia wanatakiwa wafanye biashara ya ubia kwa kusudio la faida kubwa, wawe na busara na waaminifu miongoni mwao, na kutoa mahesabu ya kweli na taarifa za vitu vyote vinavyohusu ubia kwa mbia au wawakilishi wake wa kisheria.

Haki za hiyari na wajibu wa wabia, iwe zimetajwa kwenye makubaliano au sheria ya Mikataba Sheria namba 345, zinaweza kubadilishwa kwa ridhaa ya wabia wenyewe, na ridhaa hiyo inaweza kuwa ya wazi au yakudhaniwa kulingana na shughuli husika. (kifungu cha 193)

Haki na Wajibu wa Wabia (kifungu cha 194)

Bila ya kuwepo kwa mkataba wowote, haki na wajibu wa wadau kuhusiana na ubia zitatambuliwa kwa kanuni zifuatazo-

  1. kila mbia ana haki ya kuwa ni sehemu ya uongozi katika shughuli za ubia;
  2. tofauti yoyote itakayojitokeza katika hali ya kawaida inayohusu shughuli za ubia inaweza kuamuliwa na wabia walio wengi, lakini hakutafanywa mabadiliko yoyote kuhusiana na ubia katika biashara bila ya ridhaa ya wabia wote waliopo;
  3. kila mbia ana haki ya kuon, kukagua na kunakili kitabu chochote cha shirika;
  4. Mbia hatastahili ujira kwa kushiriki katika kutimiza shughuli za shirika;
  5. Wabia wote wanastahili kugawana sawa mtaji na faida ya biashara, na kuchangia sawa penye upotevu wa shirika;
  6. Shirika litamrejeshea kila mbia malipo na gharama zingine alizoingia-
  7. katika mazingira ya kawaida ya biashara za shirika; na
  8. kitu chochote cha msingi kilichofanywa kunusuru biashara au mali za shirika;
  9. Mbia atafidia shirika hasara yoyote atakayoisababisha kwa udanganyifu au uzembe wa makusudi katika kutekeleza shughuli za shirika.

MAJUKUMU YA WABIA KATIKA MALI ZA UBIA, FAIDA BINAFSI NA YA BIASHARA

  1. Kutunza Mali za Ubia; kwa mujibu wa Kifungu cha 195.-(1) Mali zote na haki na maslahi dhidi ya mali zilizoletwa kwenye stoo ya ubia au ailizopatikana kwa kununua au vinginevyo, kwa niaba ya shirikai, kwa sababu au kwa manufaa ya ubia, ikiwemo nia njema ya biashara, ni mali za ubia na lazima zitunzwe na wabia kwaajili ya ubia wao kulingana na makubaliano ya ubia au vifungu vya sheria hii.
  2. Labda iwe kuna nia nyingine, mali na haki na maslahi dhidi ya mali iliyopatikana kwa pesa ya shirika vitahesabiwa kuwa vimenunuliwa kwa akaunti ya shirika.
  3. Ikiwa aridhi au mali yoyote inayoweza kurithiwa imekuwa ni mali ya ubia, kama kutakuwa na nia ingine, vitashughulikwa miongoni mwa wabia (ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa wabia waliofariki), na pia kati ya warithi na wasimamizi. Jukumu la wabia katika faida binafsi na ya biashara

Kuwa mkweli na muwazi katika biashara; fanya marejeo kifungu cha 196. Kufuatana na uwepo wa mkataba baina ya wabia-

(a) iwapo mbia anapata faida yoyote kutokana na shughuli za shirika, au kutokana na kutumia mali au biashara inayolihusu shirika au jina la shirika, anatakiwa ajulishe faida aliyopata na kulipa shirika;

(b) Ikiwa mbia anafanya biashara inayofanana au kushindana na shirika, bila ya kuwa na ridhaa ya wabia wengine, atataja faida na kulilipa shirika kwa faida yote aliyoipata katika biashara.