Skip to main content

Mikopo inayohusisha uwekaji wa Dhamana

Sheria ya Mikopo inayohusiana na kuweka mali rehani inatambulika kama Fedha (Masharti Maalum) Sheria ya mwaka 2008 (Mortgage Financing (Special Provision) Act 2008). Sheria hii ilitungwa kwa kufanya marekebisho na kufuta baadhi ya vifungu kwenye sheria ya Ardhi sura Namba 113 pamoja na sheria ya usajili wa Ardhi Sura Namba 334 kuweka katika hali nzuri ya namna mwananchi anaweza kuweka mali yake rehani kwa utaratibu mzuri. Mfano wa mali zinazoweza kuwekwa kama rehani ni kama vile Nyumba, Ardhi au kitu chochote kisichohamishika. Pia itambulike kwamba uwekaji wa rehani mali kwa unaowekwa na mjasiliamali au mtu yeyote, au shirika au kampuni ni jambo ambalo linapelekea athari fulani ya kushuka na kupanda kwa uchumi Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla.

Mkopaji ni nani?

Mkopaji ni mtu yeyote ambaye ni mwananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, ambaye ana mali ya kuweka rehani, amabayo inathamani sawa au zaidi na mkopo anaotaka kukopa lakini pia mwenye wadhamini.

Wajibu wa Mkopaji

Mkopaji anatakiwa kufanya mambo yafuatayo pale anapokutana na mkopeshaji, kwa ajili ya kukopa.

  1. Mkopaji ana wajibu wa kuweka wazi kama kweli ana mke au mume kwa nyaraka mfano cheti cha ndoa, au nyaraka zozote zinaoonesha uwepo wa mke au mume kwa mkopaji husika. Baada ya hapo mkopeshaji anawajibu kwenda kuchunguza kwa mkopaji kama kweli kinachozungumzwa ni cha kweli au cha uongo.
  2. Mkopaji anatakiwa kumridhisha mkopeshaji kwa kuwasirisha kiapo cha kuwa ana mke. Sio tu kuwasirisha kiapo mkopeshaji anatakiwa kujiridhisha juu ya hicho kiapo.

Nini kitatokea pale ambapo mkopaji ataleta nyaraka za uongo.

Pale ambapo mkopaji atatoa taarifa au nyaraka za uongo, kitendo hicho ni kosa la jinai. Ambapo mkopaji atalazimika kulipa nusu ya gharama ya mkopo ambao alikuwa anaomba kutoka kwa mkopaji au kufungwa kifungo kisichopungua miezi kumi na miwili (12). Hivyo basi ni vizuri mkopaji akatoa taarifa za kweli ili kuweza kuepuka adhabu hiyo.

Nini kitatokea pale ambapo mkopaji ana ndoa na ameshindwa kumhusisha mwanandoa mwenzake.

Pale ambapo mkopaji ameshindwa au ameficha kuonesha kuwa ameoa, na akafanikiwa kupata mkopo huo, kitakachotokea ni kwamba, huo mkopo utakuwa batili. Kwa sababu rehani inahusisha mali ambazo mara nyingi zinakuwa ni mali za familia na kisheria ni lazima ridhaa ya mume au mke itolewe kabla yakutoa mkopo. Kama mkopo ukishindikana kulipwa mali iliyowekwa rehani itauzwa ili kuweza kufidia mkopo huo.. Hivyo basi bila kuwa na taarifa kwa mwana ndoa mwingine itakuwa ni kosa kulipa gharama au kuwajibishwa kwenye kitu amabacho hana taarifa nacho wala hakuusika kufanya kosa lile. Kwa hiyo sheria hiyo ipo kwa ajili ya kuhakisha kwamba wana ndoa wote wawili wanahusika kwenye kulipa mkopo husika.

Ila ijulikane pia kuwa hata mtu ambaye hana ndoa, au hajaoa, au alipewa talaka au alitoa talaka, kwa maneno mengine hana ndoa inayotambulika kwa sheria ya ndoa pamoja na sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtu huyo anayo haki ya kuomba mkopo bila kujali jinsia, sura, kabila, rangi na sehemu atokako kwenye taasisi yoyote inayotambulika kisheria ndani ya Tanzania.

Nini kitatokea pale amabapo, mkopaji atashindwa kulipa mkopo.

Kwa mujibu wa sheria mkopeshaji lazima kumuandikia taarifa (Demand Notice/Letter) kwa mkopaji kumtaarifu kuwa, muda wa kurejesha mkopo umeisha, anaweza kupewa muda Fulani kulipa na asipolipa mali yake inaweza kuuzwa au kumilikiwa ili kufidiwa mkopo. Akishindwa kulipa atapewa tena notisi nyingine na akishindwa kulipa, ndipo mkopeshaji ataenda Mahakani kuomba mahakama ili kupewa nguvu ya kumiliki, au kuuza mali amabayo imewekwa rehani.

Ingawa ikitokea kwamba mkopaji ameweza kupata hiyo fedha hata kulipa nusu yake na kuwa na sababu za msingi za kuonyesha ni kwa nini ameshindwa kulipa mkopo huo mapema au ndani ya muda uliopangwa kwenye mkataba, anaweza kwenda Mahakami na kuomba mahakama isimpe mkopeshaji mamlaka ya kuuza, kumiliki, au kuchukua kwa namna yoyote ile mali ya mkopaji. Mahakama itapima uzito wa sababu hizo na kukubali au kukataa maombi ya mkopaji.

Kitu gani kitatokea pale amabapo mkopeshaji ameuza mali na kupata faida zaidi ya mkopo uliochukuliwa?

Ikitoteka mkopo sasa umelipwa kwa kuuza mali iliyowekwa rehani na mkopeshaji alafu kuna kiasi chochote kimebaki lazima kiwango hicho cha fedha kipelekwe kwa mkopaji kama kiwango kilichozidi kwenye mkopo wote aliokopa kulinganaa na makabuliano. Mkopaji atarudishiwa kiwango cha fedha kilichozidi baada ya kulipa madeni yote, fidia pamoja na penati zilizojitokeza kulingana na ma.

Mfano Tuchukulie kuwa

  1. MKOPAJI
  2. BENKI (MKOPESHAJI)

A kwa ruhusa ya mke wake aliweka mali yake rehani yenye thamani ya shilingi Milioni Hamsini (50,000,0000/=) ambayo ilikuwa ni nyumba ya kudumu kwa ajili ya kuchukua mkopo wa shilingi milioni ishirini (20,000,0000/=) kutoka kwa B. Ambapo pamoja na fidia ya mkopo huo A alitakiwa kurejesha mkopo wa jumla ya shilingi milioni ishirini na saba (27,000,000/=) ndani ya mwaka mmoja tu. Ikitokea A ameshindwa kurejesha mkopo pamoja na kukumbushwa kwa barua, Nyumba ikauzwa kwa thamani ya shilingi Milioni sabini (70, 000,000/=). B anatakiwa kuchukua milioni 70,000,000 – 27,000,000 kiasi kitacho baki kirudishwe kwa A sawa na Milioni Arobaini na tatu 43,000,000/=.

Na kama kuna gharama zimetumika mahakamani zinaweza kukatwa hapo amabapo huwa sio nyingi. Wananchi wengi walikuwa wanajua kwamba Ukishindwa kulipa mali uliyoweka rehani inauzwa na mkopaji hapati chochote, hapana sio kweli. Ingawa lazima fedha iliyopatikana ilipe deni na na gharama nyingine zinazoambatana na deni hilo na kiasi kinachobaki ndicho kinachorejeshwa kwa mkopaji.

Nini kitatokea pale amabapo Mali iliyowekwa rehani imeuzwa bila kufidia mkopo uliyochukuliwa na mkopaji?

Kwanza kabisa lazima tufahau kwamba kabla ya Benki au taasisi kukopesha mkopo Fulani kwa mkopaji huwa lazima atafutwe mtaalam wa kufanya tathmini aangalie mali inayokusudiwa kuwekwa rehani kwa ajili ya kujiritdisha kwa kufanya tathmini kwa kila kitu kinachohusisha mali hiyo kama ni nyumba au kiwanja. Aidha tathmini hiyo ni lazima ifanyike kulingana na gharama za wakati huo. Lakini pia ijulikane kuwa thamani ya mali hiyo inapanda thamani kulingana na uhitaji wa wakati huo na eneo lilipo.

Kwa hiyo tathmini ya mali hiyo itafanyika na kutoa taarifa ya kitaamu kwa Benki au Taasisi inayokusudiwa kukopesha fedhaa kwa mkopaji. Kukiwa na uridhishwaji juu ya taarifa hiyo au tathmini hiyo ndipo taratibu zilizowekwa zitafwatwa kisha mkopo unatolewa.

Sasa ikitokea mkopaji ameshindwa kulipa mkopo na kuikomboa mali yake, Benki au taasisi ikauza mali iliyowekwa rehani bila kufidia mkopo uliochukuliwa, hakuna mali yoyote nyingine ya mkopaji itakayouuzwa kufidia mkopo. Hii ni kwasababu kuwa mkataba uliopo lazima ndio utakao husika katika kuuza mali husika iliyoko kwenye mkataba na sio kuchukua mali nyingine ya mkopaji. Hivyo basi kitakachotokea hapa ni kwamba, Benki au taasisi husika itakuwa imepata hasara yenyewe.